Wachezaji wa timu za Ruvu
Shooting wenye jezi rangi ya bluu na wa African Lyon wakiwa wamelala
chini ikiwa ni kujihami na makundi ya nyuki ambayo yalikuwa yanapita
uwanjani hapo hivyo wachezaji, waamuzi na mabenchi ya wachezaji wa
akiba wote walilazimika kulala chini ikiwa ni kujinusuru kutokana na
hali hiyo. Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Shooting iliibuka na ushndi wa bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji
mwenye nguvu za miguu Issa Kanduru kunako dakika ya 19.
Refa na wachezaji wakiwa wamekimbia
kutoka uwanjani kuwakimbia nyuki waliovamia uwanja ghafla
Benchi la ufundi na baadhi ya wachezaji pamoja na msaidizi wa refa wakiwa wamelala chini kuepuka nyuki hao
Nyuki si mchezo kila mtu alilala chini na kutibua kwa muda mechi hiyo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni