Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Hoyce Temu akitoa semina juu ya Malengo endelevu ya umoja wa mataifa katika Chuo Kikuu cha Tumaini
University Makumira kilichopo mkoani Arusha
Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini Amon manyama akifafanuajambo juu ya Malengo endelevu ya umoja wa mataifa katika Chuo Kikuu cha Tumaini University Makumira kilichopo mkoani Arusha
Na Woinde Shizza,Arusha
Maafisa kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) wamefanya ziara ya
kutembelea chuo cha Tumaini University tawi la Arusha ikiwa ni pamoja na
kutoa semina juu ya Malengo endelevu ya umoja wa mataifa ikiwemo kufuta
umasikini,kuondoa njaa na kuhakikisha upatikanaji wa maji.
Program Specialist wa UNDP ,Amon Manyama amesema kuwa Wasomi na wanafunzi walioko vyuoni wanapaswa kuelewa vizuri malengo endelevu ya umoja wa mataifa ili waweze kuyatimiza katika ngazi zao hasa ukizingatia kuwa wanachuo ni Wataalamu watarajiwa,na viongozi wa kesho.
Manyama amesema kuwa taasisi,mashirika na jamii pamoja na serikali ina
jukumu kubwa la kutekeleza malengo hayo ili kuondoa umasikini,kujenga
uchumi endelevu,kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano UN ,Hoyce Temu amesema kuwa vijana hususan Wanavyuoni wanapaswa kuwa mambalozi wazuri wa kuyatangaza malengo endelevu ya UN ili yaweze kutimia na dunia iwe ni sehemu bora zaidi ya kuishi.

Hoyce amesema kuwa UN ina mpango wa kuwafikia vijana walioko vyuoni na
mitaani ili waweze kuelewa vizuri juu ya malengo 17 ya Umoja wa mataifa na
kujua jukumu walilonalo ndani ya malengo hayo.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni