.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 14 Januari 2017

BALOZI SEIF AKUTANA NA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA TANZANIA, JENERALI DAVIS MWAMUNYANGE

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akibadilishana mawazo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange akipokea zawadi ya Mlango kutoka kwa Balozi Seif kama ishara ya utumishi wake uliotukuka kwa jinsi alivyolitumikia Jeshi la Wananchi kwa nidhamu takriban miaka 45.
Jenerali Mwamunyange akiaga rasmi kwa Balozi Seif baada ya kumaliza mazunguimzo yao. Picha na – OMPR – ZNZ.

Jeshi la Wananchi wa Tanzania { JWTZ } limeelezea faraja yake kutokana na juhudi kubwa zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuwaletea Maendeleo Wananchi wake bila ya bila ya kuingizwa cheche za kibaguzi.

Faraja ya Jeshi hilo imekuja kufuatia ushuhuda wa Taasisi za Kimataifa zinavyothibitisha maendeleo makubwa yaliyofikiwa na wananchi wa Zanzibar na kubadilisha ustawi na uchumi wao ndani ya kipindi cha zaidi ya miaka 50 iliyopita.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama Tanzania General Davis Mwamunyange wakati akiwasilisha salamu za pongezi za Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutokana na kufanikisha vyema sherehe za Maadhimisho ya kutimia miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

General Mwamunyange alisema ongezeko la miradi ya maendeleo iliyoanzishwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiambatana na Miundombinu imara inayowekwa katika maeneo mbali mbali ya Visiwa vya Unguja na Pemba imewawezesha wananchi mbali mbali kuwa na uhakika wa kuendesha maisha yao ya kila siku.

Alisema Visiwa vya Zanzibar hivi sasa vimebadilika kiuchumi pamoja na kibiashara kiasi cha kuzioa harakati za kibiashara na kimaisha kuongezeka zaidi zinazotoa fursa kwa wawekezaji wa nje ya Zanzibar kuanzisha miradi yao inayosaidia kuongeza pia fursa za ajira hasa kwa kundi la Vijana.

Akizungumzia migogoro ya Ardhi inayojichomoza kati ya Wananchi na Kambi za Jeshi hilo ziliopo jirani na maeneo yao Mkuu huyo wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania alisema Uongozi wa Jeshi hilo utaandaa utaratibu maalum wa kuyaachia baadhi ya maeneo ya ardhi ambayo hayana umuhimu kwa shughuli za kiulinzi ili yatumiwe na Wananchi kwa shughuli zao za Kimaisha.

General Devis Mwamunyange alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba mahitaji ya ardhi kwa sasa hapa Nchini yamekuwa makubwa kutokana na ongezeko kubwa la Idadi ya Watu pamoja na kubadilika kwa harakati za Kiuchumi.

Aliwashukuru Wananchi wa maeneo yaliyoibuka migogoro hiyo kuendelea kuwa wastahamailivu na kuipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa juhudi iliyochukuwa ya kusaidia kutafuta suluhu ya migogoro hiyo jambo ambalo limesaidia kuleta hali ya utulivu na amani katika maeneo hayo.

Akitoa shukrani zake kwa kazi kubwa ya ulinzi inayoendelea kufanywa na Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema nidhamu na Heshima iliyojengeka ndani ya vikosi hivyo vimeiwezesha Tanzania kuwa na heshima Kimataifa.

Balozi Seif alisema Umoja wa Mataifa { UN } umekuwa ukikimbilia Tanzania kutaka nguvu za ulinzi isaidie kwenye maeneo ya Mataifa yenye migogoro ya kisiasa na kiusalama baada ya kubaini nidhamu kubwa iliyopo ndani ya Jeshi la Tanzania.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Vikosi vya Ulinzi Tanzania vimekuwa na uwezo, nguvu, uzoefu na nidhamu kubwa ya kusimamia ulinzi wa Taifa na haya yamepatikana kutokana na mafunzo wanayopewa na Wataalamu pamoja na Viongozi wao.

Balozi Seif alitmia mkutano huo kuwasilisha salamu za pole kwa Uongozi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kufutia kifo cha Kamanda wa Brigedia ya Nyuki Zanzibar Brigedia Generali Cyrill Ivor Mhaiki.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni