Mabingwa mara nne timu ya Cameroon
wamekwea juu ya kundi A baada ya kupambana na kuinyima wageni katika
michuano hiyo Guinea-Bissau ushindi wa kihistoria kwenye Michuano wa
Mataifa ya Afrika.
Guinea-Bissau, iliushtua ulimwengu
wa soka Afrika baada ya kuongoza kufunga goli kupitia jitihada
binafsi za mchezaji Piquito, lakini Cameroon wakasawazisha katika
kipindi cha pili kupitia kwa Sebastien Siani.
Cameroon waliongeza goli la pili
kupitia kwa shuti la chini la Michael Ngadeu-Ngadjui, na kufanya
mchezo huo kumalizika kwa matokeo ya magoli 2-1. Katika mchezo wa
awali wenyeji Gabon walitoka sare ya 1-1 na Burkina Faso.
Pierre-Emerick Aubameyang akiwa ameshika mpira baada ya kufunga goli kwa penati
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni