Mshambuliaji Diego Costa ameachwa
kwenye kikosi cha Chelsea kitakachoivaa Leicester hii leo baada ya
kutofautiana na kocha wake kuhusiana na kuwa fiti.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa
Hispania hakuwepo kwenye mazoezi kwa siku tatu, na hajasafiri kwenda
na timu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Leicester.
Taarifa hizo zimekuja huku kukiwa na
ripoti ya kuwepo kwa ofa ya kwenda kuchezea China, ambapo Costa
atachuma kiasi cha paundi milioni 30 kwa mwaka.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni