Everton imeonyesha mchezo mzuri na
kuiduwaza Manchester City kwa kuipatia kipigo kikali cha magoli 4-0,
ambacho ni pigo katika harakati za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya
Uingereza.
Everton waliweza kudhibiti umiliki
wa asilimia 71 wa Manchester City, kwa kutumia vyema nafasi nne
kufunga goli kati ya sita walizopata.
Romelu Lukaku alifunga goli la
kwanza kufuatia pande la Kevin Mirallas na kisha baadaye Lukaku
akishirikiana vyema na Mirallas ambaye aliachia shuti na kufunga goli
la pili.
Tom Davies aliibua shangwe katika
dimba la Goodison Park baada ya kufunga goli katika sekunde chache
tangu aingie dimbani kwa mara ya kwanza akicheza mchezo wa ligi kuu,
na Ademola Lookman akafunga.
Romelu Lukaku akiwa ameachia shuti lililoandika goli la kwanza la Everton
Maumivu ya kichwa huanza taratibu: Silva akiwa ameshikilia kichwa akisikilizia maumivu ya kufungwa
Kocha Pep Guardiola naye mkono kichwani, kipigo si mchezo leo ni mwendo wa panadol tu
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni