Kocha Jose Mourinho amegoma kukubali
kuwa rekodi ya Manchester United kucheza michezo 17 bila kufungwa
imetibuliwa baada ya kufungwa magoli 2-1 na Hull City katika mchezo
wa kombe la EFL.
Kocha huyo aliyepigwa picha akiwa na
chupa ya wine na keki ya kutimiza miaka 54 ya kuzaliwa, anaamini kuwa
Manchester United sasa wamecheza michezo 18 bila ya kufungwa.
Hii nikutokana na kocha huyo Mreno
kutokubali goli la penati la Hull, alilofunga Tom Huddlestone, baada
ya refa Jon Moss kusema beki Marcos Rojo alimvuta jezi Harry
Maguire.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni