Kipa wa Misri Essam El-Hadary
amekuwa mchezaji mwenye umri mkubwa kucheza katika michuano ya kombe
la Mataifa ya Afrika, na kuisaidia timu yake ya Misri kutoka sare
tasa na Mali.
El-Hadary ambaye amefikisha miaka 44
siku ya jumapili aliingia dimbani katika kipindi cha kwanza baada ya
kipa Ahmed El-Shenawy, aliyejigonga kwenye mwamba wa goli wakati
akiokoa krosi ya Moussa Marega.
Mchezaji wa Arsenal na Mirsi Mohamed
Elneny alipoteza nafasi mbili za Misri kufunga katika kipindi cha
kwanza kwa kupiga mpira juu ya goli na na nyingine kuupiga mpira nje
kabisa ya goli.
Katika mchezo mwingine timu pekee
kutoka mataifa ya Afrika Mashariki katika michuano hiyo Uganda,
ilijikuta ikifungwa goli moja kwa bila na Ghana, goli ambalo
lilifungwa kwa mkwaju wa penati na Andrew Ayew.
Andrew Ayew wa Ghana akikimbia wakati akishangilia goli la penati alilofunga
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni