Mshambuliaji wa Liverpool, Sadio
Mane, amefunga goli wakati Senegal ikiifunga Zimbabwe na kuwa timu ya
kwanza kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika
2017.
Katika mchezo huo Sadio Mane
alifunga goli la kwanza kwa shuti la karibu katika dakika ya tisa
akiunganisha pasi ya mchezaji wa Lazio, Keita Balde Diao.
Mchezaji Henri Saivet, anayecheza
kwa mkopo St Etienne akitokea Newcastle, alifunga goli zuri la pili
kwa shuti la yadi 20, dakika nne tu kupita tangu kufungwa goli la
kwanza.
Katika mchezo wa awali hapo jana
Tunisia imejiweka katika nafasi nzri ya kusonga robo fainali ya
michuano hiyo baada ya kuwafunga majirani zao Algeria magoli 2-1.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni