Afisa Mkuu wa Ufundi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw Senzige Kisenge (aliyenyoosha mkono), akitoa maelezo ya Utendaji wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Prof Makame Mbarawa (Katikati) alipotembelea Makao Makuu ya TTCL leo jijini Dar es Salaam.Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Prof Makame Mbarawa (Wa pili kushoto) akizungumza na baadhi ya wateja wa TTCL waliotembelea Kituo cha Huduma kwa Wateja kilichopo Makapo Makuu ya Kampuni hiyo mara baada ya kukitembelea Kituo cha Serikali cha Kuhifadhia Data na Kumbukumbu (NIDC) kilichopo kijitonyama Jijini Dar es Salaam leo. Pichani ni Muonekano wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano unavyofanya kazi.Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Profesa Makame Mbarawa akizungumza na menejimenti ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) leo alipotembelea Makao Makuu ya TTCL na Kituo cha Serikali cha Kuhifadhia Data na Kumbukumbu (NIDC) kinachoendeshwa na kampuni ya TTCL.Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kulia) akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Prof Makame Mbarawa (hayupo pichani) alipotembelea Makao Makuu ya TTCL leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha wa TTCL, Prygod Kimweri. Baadhi ya maofisa waandamizi wa TTCL wakiwa katika mkutano huo na waziri.Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA toka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Bi. Nikusubila Maiko (wa kwanza kulia) akiwa katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni Meneja Ufundi wa NIDC, Kironde Kaijage pamoja na Katibu wa Waziri Prof. Makame Mbarawa wakiwa katika mkutano huo.
SERIKALI imezitaka taasisi zake kote kuachana na mpango wa kujenga Vituo binafsi vya vya kuhifadhia kumbukumbu (Data Center) na badala yake kutumia Kituo cha Serikali cha kuhifadhia Data na kumbukumbu (NIDC) chenye uwezo na hadhi ya Kimataifa. Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Profesa Makame Mbarawa baada ya kufanya ziara ya kutembelea kituo hicho cha Kimataifa cha kuhifadhia kumbukumbu za kimtandao na Makao Makuu ya Kampuni ya Simu Tanzania TTCL.
Mheshimwa Mbarawa amesema, Serikali imetumia fedha nyingi sana kujenga miundo mbinu ya kituo hicho mahiri katika eneo lote la Afika Mashariki na kusisitiza kuwa, Taasisi za Serikali ni lazima zitumie kituo hicho na kwa zile zenye mpango wa kujenga vituo binagsi, ziachane na mpango huo ambao ni matumizi mabaya ya fedha za Umma.
'Natoa agizo kwa taasisi zote za Umma, ziachane kabisa na mpango wa kujenga Data Centres. Serikali imebeba jukumu hilo, imejenga kituo cha hadhi ya juu kabisa, sote tukitumie kituo hiki. Kila taasisi zijikite katika majukumu yao ya msingi, hili la Data Centre watuachie Serikali kwa kuwa tumeshalitekeleza, hatuwezi kuendelea kutumia fedha nyingine kwa eneo hili, tuelekeze fedha hizo katika maeneo mengine muhimu.'
Akiwa katika Makao Makuu ya Kampuni ya Simu nchini TTCL, Mhe Mbarawa ameitaka Menejimenti ya Kampuni hiyo kuongeza kasi ya utendaji kazi na ubunifu ili kukabiliana na ushindani uliopo katika sekta hiyo sambamba na kukidhi kiu ya Wananchi ya kupata huduma Shirika lao.Mkuu wa Kituo cha Serikali cha Kuhifadhia Data na Kumbukumbu (NIDC), Abdul Mombokaleo (kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Profesa Makame Mbarawa (kushoto) alipotembelea kukagua utendaji kazi wa kituo hicho.
'TTCL mna deni kubwa kwa Wananchi. Tumeondoa vikwazo vingi vilivyokuwa vikiwakwamisha na sasa tunataka kuona kasi ya uhakika ya utendaji kazi. Tumewalipa Bharti Airtel na kuvunja ubia nao, tumewafutia madeni, tumewakabidhi Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na Kituo cha Kimataifa cha kuhifadhia kumbukumbu mviendeshe kwa niaba ya Serikali.
Yote haya yamefanyika kwa nia moja ya kuwajengea uwezo ili mtimize majukumu yenu vizuri.' amesema Waziri Mbarawa. Katika hatua nyingine, Waziri Profesa Mbarawa amepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na TTCL katika kuboresha huduma zake nchini. Aidha, Mhe Mbarawa ameeleza kuridhika kwake na kasi kubwa ya kusambaza huduma za mtandao wa 4G LTE na kujitangaza zinazofanywa na Kampuni hiyo katika maeneo mbali mbali nchini.
Awali katika taarifa yake fupi kwa Mhe Waziri, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw Waziri Kindamba amesema, hadi kufikia Januari 16, 2017 Mikoa 7 ya Tanzania bara inapata huduma kwa teknolojia ya 4G LTE ambayo ni Dar es Salaam, Dodoma, Pwani, Morogoro,Mwanza, Mbeya na Arusha. Tarehe 11 Januari 2017, siku moja kabla ya maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, TTCL ilizindua huduma za 4G LTE mjini Unguja.
Bw Kindamba ameongeza kuwa, kutokana uhusiano wa shughuli za kiuchumi na kijamii baina ya Visiwa vya Unguja na Pemba, TTCL inakusudia kupeleka huduma za 4G LTE Kisiwani Pemba katika muda mfupi ujao ili kulifanya eneo lote la Tanzania Visiwani kufikiwa na huduma na kusaidia katika ukuaji wa shughuli za kiuchumi,huduma za kijamii,ulinzi na usalama katika maeneo hayo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni