Ngumi zimerushwa bunge nchini Afrika
Kusini kufuatia wabunge wa upinzani kugoma kutolewa nje ya bunge
wakati wakijaribu kumzuia rais Jacob Zuma kuhutubia taifa.
Wabunge wa chama machachari cha
upinzani cha EFF, kinachoongozwa na Julius Malema wakiwa wamevalia
nguo nyekundu walipambana na walinzi wa bunge waliokuwa wakiwatoa nje
ya ukumbi wa bunge.
Baada ya hapo polisi tena
walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa vyama
vya upinzani na wa serikali ambao walihamishia mapambano hayo nje ya
ukumbi wa bunge.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni