Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakati alipokwenda kwenye Ofisi kuu ya ATCL kufuatilia mwenendo wa uendeshaji wa Shirika na usimamizi wa mapato , Februari 9, 2017. Kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Profesa Makame Mbarawa na kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Regini Masoud (kulia) kuhusu mfumo mpya wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki wakati alipotembelea ofisi kuu ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) jijini Dar es salaam kufuatilia mwenendo wa uendeshaji wa Shirika na usimamizi wa mapato, Februari 9, 2017. Kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Profesa Makame Mbarawa na kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Ametoa kauli hiyo leo (Alhamis, Februari 9, 2017) alipotembelea Makao Makuu ya shirika hilo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujionea mwenendo wa uendeshaji wake.
“Nitamuagiza CAG aje aangalie mwenendo wa ukusanyaji wa mapato ya shirika hili kuanzia mwaka jana lilipoanza kufanya kazi hadi sasa,” amesema.
Waziri Mkuu amesema Serikali haiko tayari kuona shirika hilo linakufa tena, hivyo amewataka viongozi wake wahakikishe linaendeshwa kwa mafanikio kwa manufaa ya Taifa.
Pia amewataka waache kukusanya mapato kwa kutumia risiti za kuandika kwa mkono na badala yake waanze kutumia mfumo wa kieletroniki ili kuzuia upotevu wa mapato hayo.
“Vitu vingi vinavyoenda manual ni rahisi kufa. Serikali tumeagiza malipo yote yafanyike kielektroniki na kote tunakotumia mfumo huu tumepata mafanikio,”amesema.
Katika hatua nyinginre, Waziri Mkuu amemtaka Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Bi. Witness Mbaga ajiridhishe na fedha zinazokusanywa katika eneo la mizigo kama ziko sahihi, lengo ni kudhibiti upotevu wa mapato.
Hata hivyo Waziri Mkuu amewataka viongozi wa shirika hilo kuhakikisha wanazingaria ratiba ya njia na muda wa safari ili wasipoteze wateja.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
ALHAMIS, FEBRUARI 9, 2017
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni