Aliyekuwa mchezaji wa Sunderland
mshambuliaji, Asamoah Gyan, ni miongoni mwa wachezaji 40, wanaoelezwa
kuwa na ukataji nywele usioendana na maadili chini ya miongozo ya
Chama cha Soka cha Umoja wa Nchi za Kiarabu (UAEFA).
Mchezaji huyo raia wa Ghana mwenye
umri wa miaka 31 anacheza kwa mkopo huko Dubai katika Ligi ya Ghuba
kwenye klabu ya Al Ahli, akitokea timu ya Shanghai SIPG.
Baadhi ya maandiko ya dini ya
Kiislam yanakataza ukataji nywele kwa mitindo mbalimbali, ambapo sasa
maafisa wa Umoja wa Mataifa ya Kiarabu wanataka kuzuiwa wachezaji ukataji
nywele wa mitindo ili kuepusha watoto kuiga.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni