.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 10 Februari 2017

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFANYA KIKAO NA WAFANYAKAZI WA WIZARA YAKE

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akizungumza na Wafanyakazi wa Wizara yake wa Fungu 51 kuhusu masuala mbalimbali ya kiutendaji. Kikao hicho ambacho kinafanyika mara mbili kwa mwaka kimeandaliwa na Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), (hawapo pichani). Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya na Mwenyekiti wa chama hicho, William Mkombozi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya, akizungumza na Wafanyakazi wa Wizara yake wa Fungu 51 kuhusu masuala mbalimbali ya kiutendaji. Kikao hicho ambacho kinafanyika mara mbili kwa mwaka kimeandaliwa na Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), (hawapo pichani). Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), Tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, William Mkombozi akizungumza na Wafanyakazi wenzake wa tawi hilo (hawapo pichani), wakati wa mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa akijibu baadhi ya hoja zilizoelekezwa kwenye idara yake wakati wa mkutano wa Wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), katika mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mjumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), Tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwanaidi Shabaani akiuliza swali kwa Katibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (hayupo pichani), wakati wa mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO

SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni