Mwanasheria maarufu wa haki za
binadamu, Amal Clooney, na mumewe muigizaji nyota wa filamu George,
wanatarajia kupata watoto mapacha.
Watoto hao wa wanandoa hao mashuhuri
wanatarajiwa kuuona ulimwengu mwezi Juni, mwaka huu kwa mujibu wa
mtangazaji wa kipindi cha maongezi cha CBS, Julie Chen.
Chanzo kingine kimoja kilichopo
karibu na wanandoa hao, kimesema wanafuraha mno, hata hivyo
wawakilishi wa familia hiyo ya Clooney hawajasema chochote.
Hivi karibuni wanandoa nyota wa
muziki Marekani Beyonce na mumewe Jay-Z nao walitangaza kuwa nao
wanatarajia kupata watoto mapacha, hii inaashiria kuwa mwaka huu ni
wa mastaa kujaliwa watoto mapacha.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni