Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool,
Mfaransa Djibril Cisse, ametangaza kujiuzulu kusakata soka akiwa na
umri wa miaka 35 na kujitumbukiza katika sekta ya burudani.
Cisse, ambaye pia aliwahi zichezea
timu za Sunderland na QPR za Uingereza, sasa atatenga muda wake
katika ajira yake mpya ya u-DJ na utengenezaji nguo zake za 'Mr
Lenoir'.
Cisse ambaye alitangaza kujiuzulu
soka Oktoba mwaka 2015, baada ya kushindwa kupona kwa muda mrefu
majeraha, alirejea soka mwaka jana baada ya kufanyiwa upasuaji.
Mfaransa Djibril Cisse akiwa katika majukumu ya U-DJ
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni