.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 10 Februari 2017

RIPOTI YA TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR YAKABIDHIWA KWA DK. SHEIN

OTH
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea Ripoti ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar ya mwaka 2015 kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Mhe,Jecha Salim Jecha (kushoto) katika hafla fupi iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
OTH 3
 Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe,Jecha Salim Jecha (kulia) akitoa maelezo mafupi kabla ya kukabidhi Ripoti ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar ya mwaka 2015 hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja. 
OTH 4
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa kizungumza na mawaziri mbali mbali,watendaji wa Serikali (hawapi pichani), Wajumbe wa Tume ya uchaguzi baada ya kukabidhiwa Ripoti ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar ya mwaka 2015 na Mwenyekiti wa Tume hiyo Mhe,Jecha Salim Jecha (katikati) katika hafla fupi iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 09/02/2017.
OTH 1
 Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Washauri wa Rais waliohudhuria katika hafla ya kukabidhiwa Ripoti ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar ya mwaka 2015 kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Mhe,Jecha Salim Jecha (hayupo pichani) katika hafla fupi iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
OTH 2
 Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu (kushoto) na Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa Ripoti ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar ya mwaka 2015 kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Mhe,Jecha Salim Jecha (hayupo pichani) katika hafla fupi iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni