Wanandoa nchini Kenya waliofunga
ndoa iliyogharimu shilingi 100 tu ya Kenya, wamerejea kiapo chao cha
ndoa yao jana katika Siku ya Wapendanao katika sherehe kubwa
iliyoandaliwa na wasamaria wema.
Habari za wanandoa hao zilisambaa
kwenye mitandao ya jamii mwezi uliopita nchini Kenya na watu wengi
walioguswa na tukio hilo waliamua kujitolea kuigharamia upya tena
harusi yao hiyo ili iwe ya kumbukumbu.
Katika harusi ya kwanza wanandoa hao
Wilson na Ann Mutura walifunga ndoa wakiwa wamevalia nguo za kawaida
fulana na jinzi, na kuvishana pete za chuma kanisani. Harusi yao ya
marejeo iliyofadhiliwa inakasiwa kugharimu dola 35,000.
Wanandoa Wilson na Ann Mutura wakifunga ndoa yao ya awali iliyogharimu kiasi cha sh 100 za Kenya sawa na sh 1,800 za Tanzania
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni