Uingereza imepata ushindi wa magoli
2-0 dhidi ya Lithuania katika mchezo wa kuwania kufuzu kutinga
michuano ya kombe la Dunia.
Katika mchezo huo Jermain Defoe
alifunga goli lake la kwanza tangu arejee kimataifa baada ya miaka
minne naye Jamie Vardy akafunga goli la pili dakika sita tangu aingie
dimbani.
Uingereza inaendelea kuwa na rekodi
ya kutofungwa katika kundi F, ingawa kikosi hicho cha Gareth
Southgate hakikucheza mchezo mzuri hapo jana.
Mshambuliaji Jermain Defoe akiifungia Uingereza goli la kwanza
Jamie Vardy akiifungia Uingereza goli la pili katika mchezo huo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni