Mkuu wa mkoa Simiyu Antoni Mtaka akikabidhi makepteni wa Timu ya taifa ya Riadha leo rasmi bendera ya Tanzania kwenda kuwakilisha nchi katika mashindano ya mbio za nyika za dunia yayotarajiwa kufanyika Marchi 26 nchini Uganda ,kapteni wa kike anaitwa Magdalena Krispini akiwa mkono wa kushoto ,na kapteni wa kiume Fabian Josephy akiwa mkono wa kushoto.
Na Woinde Shizza,Arusha
Timu ya taifa ya Riadha leo imekabidhiwa rasmi kupeperusha bendera ya Tanzania kwenda kuwakilisha nchi katika mashindano ya mbio za nyika za dunia yayotarajiwa kufanyika Marchi 26 nchini Uganda.
Akikabidhi bendera hiyo , Rais wa shirikisho la Riadha Tanzania ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka alisema kuwa mashindano haya ni makubwa kidunia na nchi zipatazo 70 zitashiriki mashindano haya ,pia kutakuwepo na nchi zingine 216 ambazo zitashiriki lakini hazitaleta timu.
Aidha alibainisha kuwa hii ni mara ya kwanza kwa nchi ya Tanzania baada ya miaka 26 kupita kupeleka timu ambayo imekamilika ikiwa na wachezaji 28 sawa na nchi zingine kama vile Ethiopia,Kenya na Uganda.
“Imepita miaka 26 tangu nchi yetu ya Tanzania ikipeleka wachezaji wakiwa kamili katika mashindano mbalimbali ,lakini kwa sasa hivi naweza kujivunia kwakuwa tumewafua wachezaji vya kutosha na tumepata timu kamili yenye wachezaji 28 ambao ni sawa na wenzetu wa Kenya na Ethiopia wanavyopelekaga wachezaji ivyo tunaimani kabisa kwa wingi huu lazima tutashinda na medani kurudi hapa nchini”alisema Mtaka
Alisema kuwa mashindano hayo yanaitaji mchezaji mwenyewe kuondoa tofauti alizonazo na kujituma zaidi kwani mbali na kuiwakilisha nchi lakini pia akishinda itamsaidia yeye mwenyewe kujinufaisha kwani zawadi zinazotolewa ni kubwa nazinamnufaisha mshindi.
Alisema kuwa wachezaji wamekaa kambini kwa muda mchache lakini wamejifua vya kutosha hivyo anaimani kabisa wanapoenda kushindana watashinda .
“Napenda kutumia muda huu kuwashukuru na kuwapongeza shirika la hifadhi ya Taifa (Tanapa) kwa kudhamini safari nzima ,na napenda kuahidia fedha zao hazitapotea bure bali zitawalipa pale wanariadha wetu watakapo rudi na medani ,napenda kuwaambia hakuna mchezo mwingine ambao wanaweza kuutumia kujitangaza zaidi ya riadha”alisema Mtaka
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa Tanapa Nyamakumbati Mafuru alisema kuwa wao kama Tanapa wameona michezo ni njia moja wapo na muhimu ya kutangaza utalii wetu wan chi yetu hivyo ndio maana tumeona tutumie fursa hii iliyojitokeza
“Unajua mashindano haya yanauthuriwa na watu wengi kutoka sehemu mbalimbali hivyo tumeona ni njia moja wapo ambayo tutaitumia kutangaza vivutio vilivyopo katika nchi yetu na ndio maana tumeamua kudhamini kuwapeleka timu hii ya taifa Uganda ili wakatuwakileshe na kututangaza pia “alisema Mafuru
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa Tanapa Nyamakumbati Mafuru alisema kuwa wao kama Tanapa wameona michezo ni njia moja wapo na muhimu ya kutangaza utalii wetu wan chi yetu hivyo ndio maana tumeona tutumie fursa hii iliyojitokeza
“Unajua mashindano haya yanauthuriwa na watu wengi kutoka sehemu mbalimbali hivyo tumeona ni njia moja wapo ambayo tutaitumia kutangaza vivutio vilivyopo katika nchi yetu na ndio maana tumeamua kudhamini kuwapeleka timu hii ya taifa Uganda ili wakatuwakileshe na kututangaza pia “alisema Mafuru
Naye katibu mkuu wa shirikisho la Riadha Gida Bidai alisema kuwa timu ya taifa imeondoka na wachezaji 28 pamoja na viongozi wake wote wakiwa salama na anaamani wataenda kuwaletea ushindi huko waendapo kwani wamefanya mazoezi ya kutosha
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni