Wanandoa raia wa Singapore
wamefungwa jela kwa kumnyima chakula mtumishi wao wa ndani anayetokea
Philippines.
Mtumishi huyo alipoteza kilogramu 20
sawa na asilimia 40 ya uzito wake kutokana na kunyimwa chakula
akifanya kazi kwa waajiri wake hao ambao walikuwa wakimpa mkate na
tambi kidogo.
Waajiri wake hao wanandoa
wamehukumiwa na Mahakama mmoja kifungo cha wiki tatu na mwingine
miezi mitatu.
Wengi wa wananchi wa Singapore
huajiri watumishi kutoka nchi za jirani, na matukio ya ukatili kwa
watumishi si jambo geni.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni