Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi akionyesha cheti maalum baada ya kuweka saini
yake cha kuthibitisha uzinduzi rasmi wa Mtandao wa Mabalozi wa
Usalama Bara barani Zanzibar { RSA } hapo Ukumbi wa zamani wa Baraza
la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Zanzibar, wa kwanza kutoka kulia ni
Naibu Kamishna wa Kikosi cha Usalama Bara barani Tanzania DCP Mohamed
Mpinga, Kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh.
Ayoub Mohamed Mahmoud, Waziri wa Ujenzi Balozi Ali Karume na Kamishna
wa Polisi Zanzibar { CP } Hamdan Makame.
Balozi Seif akimkabidhi cheti Naibu
Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar {ZBC } Bibi Narsa
Mohamed kutokana mchango mkubwa uliotolewa na vyombo vya habari vya
Shirika hilo wa suala la usalama bara barani.
Balozi Seif akikabidhi cheti maalum
kwa Mlezi wa Mtandao wa Mabalozi wa Usalama Bara barani wa Kanda ya
Pwani inayounganisha Tanga na Bagamoyo Bwana Nurdin Ali kutokana na
mchango mkubwa wa Taasisi hiyo uliosaidia kupunguza ajali za vyombo
vya moto Bara barani Tanzania Bara.Picha na – OMPR – ZNZ.
Press Release:-
Matukio ya uvunjifu wa sheria za
usalama Bara barani bado yanaendelea kuoteza nguvu kazi ya Taifa
wakiwemo Vijana wazee na watoto huku wengine wakiachwa na ulemavu wa
kudumu na wengi kuendelea kuwa mayatima katika maisha yao yote.
Akizindua rasmi Mtandao wa Mabalozi
wa wa Usalama Bara barani Zanzibar hapo ukumbi wa zamani wa Baraza la
Wawakilishi Kikwajuni Mjini Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibarf Balozi Seif Ali Iddi alisema hali hiyo imeendelea pia
kuleta hasara kwa Taifa kutokana na kuharibiwa kwa miundombinu ya
Bara bara na vifaa vyengine.
Balozi Seif alisema ajali za bara
barani bado zimekuwa ni tishio kwa maisha ya wannchi kutokana na
baadhi ya madereva ama kwa makusudi kutotii sheria na taratibu
zilizowekwa katika kufuata matumizi sahihi yaliyowekwa bara barani.
Alisema baadhi ya madereva hao
wamekuwa na tabia ya kuendesha vyombo vya moto kwa mwendo wa kasi
bila ya kujali watumiaji wengine mbali mbali kama watoto ambao nao
wana haki ya matumizi ya bara bara hizo.
Balozi Seif alionyesha masikitiko
yake kutokana na baadhi ya madereva husababisha ajali za kizembe
kutokana na ustaarabu wa kisasa ulioingiza wa kuendesha chombo cha
moto na huku wanazunguza na simu wakati mataifa mengine Duniani hili
wanalihesabu kuwa kosa kubwa bara barani.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
alisema uamuzi wa kuanzishwa kwa dhana hii ya mabalozi wa usalama
Bara barani hapa Zanzibar ni wa busara na kuwa wakati muwafaka
ambapo Serikali imekuwa ikichukuwa jitihada za kukabiliana na ajali
za bara barani.
Akizungumzia upande wa gari za Dala
dala Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema kipo kilio kikubwa
cha abiria kutokana na vitendo vya madereva na makonda vya
kutowafikisha katika vituo vyao walivyopangiwa.
Alisema mambo hayo yanawasumbua
abiria hasa wale wenye mahitaji maalum walemavu ambayo yanakwenda
kinyume na sheria za usalama bara barani pamoja na kanuni zake.
Balozi Seif alieleza kwa kutumia
utaratibu wa Mabalozi wa Usalama Bara barani wakati umefika wa
kukabiliana na matukio kwa kuwapa Taarifa kwa wakati na kuchukuliwa
hatua dhidi ya watu wote wanaohusika kuvunja sheria za Nchi.
Jeshi la Polisi usalama Bara barani
pamoja na mamlaka nyengine ni vyema likashirikiana kwa karibu na
Mabalozi wa Usalama Bara barani kwa kusimamia vyema dhana hii kwa
kutumia mikakati tofauti itakayowanasa wapinda sheria za usalama bara
barani.
Alisema kupaza sauti, kukemea pamoja
na kuchukuwa hatua nyengine kwa wale madereva watukutu kutasaidia
kuondoa udumbufu na kero zinazotokana na tabia hiyo mbaya ndani ya
Jamii.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
alilinasihi jeshi la Polisi kujenga utamaduni wa kuficha siri kwani
ni dhambi kubwa iwapo taarifa za uvunjaji wa sheria bara barani
zinazotolewa na Mabalozi kwa jeshi kutolewa kwa wavunja wa sheria
hizo.
Balozi Seif alifafanua kwamba huo ni
usaliti wa wazi na kamwe hautokubalika kwa sababu ni adui wa
maendeleo.
Mapema akitoa Tarifa Mwenyekiti wa
Mtandao wa Mabalozi wa Usalama Bara barani Nd. Justafa Mussa alisema
Mtando huo wa Kiraia umeanzishwa kwa lengo la kulisaidia Jeshi la
Polisi Kikosi cha usalama bara barani kupambana na na makosa
yanayotokana na bara bara.
Nd. Mustafa alisema dhana hiyo ya
Mabalozi wa usalama bara barani inafaa kuungwa mkono ya washirika
mbali mbali huku wakielewa kwamba jukumu la kulinda usalama wa raia
linamuhusu na kumgusa kikla mwana Jamii.
Alisema wanajumiya hao tayari
wameshaanza kutoka mafunzo kwa wanafunzi katika maskuli mbali mbali
nchini sambamba na kuwataka wana jamii kutowaonea haya madereva na
makonda wajeuri.
Naye Mlezi wa Mabalozi wa usalama
Bara barani Msaidizi Kamishna wa Jeshi la Polisi { ACP } Mkadam
Khamis Mkadam alisema ajali nyingi zinazotokea Bara barani kutokana
na vitendo visivyotii usalama bara barani.
ACP Mkadam alisema kikosi cha
usalama Bara bara kimekuwa kikibuni mbinu mbali mbali za kusimamia
usalama sambamba na kupunguza ajali kwa kiwqango kikubwa kadri
inavyowezekana.
Alisema ajali za bara barani
zilizotokeza mwaka 2016 zilifikia mia 604 na kusababisha vifo vya
watu 147 wakati mwaka 2017 uliripotiwa ajali mia 517 zilizosababisha
vifo vya watu 133 kukiwa na upungufu wa vifa vya watu 14.
Uzinduzi wa Mtandao wa Mabalozi wa
Usalama Bara barani Zanzibar ulioambatana na michezo ya kuigiza
yenye mnasaba na tukio hilo umeshuhudiwa na wanamtandao wa Mabalozi
wa usalama Bara barani kutoka Tanzania Bara wakiongozwa na Naibu
Kamishna wa Usalama Bara barani Tanzania ACP Mohamed Mhina.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar
19/4/2017.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni