Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), inatarajiwa kukutana Jumanne Aprili 18, 2017 kwa lengo la kupitia uamuzi uliofanywa na Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji Ligi Tanzania maarufu kwa jina la Kamati ya Saa 72.
Kwa mujibu wa Katiba ya TFF, Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, ina mamlaka ya kutafsiri sheria na kanuni za mpira wa miguu nchini kama ilivyoainishwa kwenye katiba na sehemu ya utangulizi ya kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
http://tff.or.tz/news/857-kamati-ya-katiba-sheria-na-hadhi-za-wachezaji-kukaa-jumanne
CAF YAPTISHA VIWANJA VYA UHURU, CCM KIRUMBA KUTUMIKA KIMATAIFA
Shirikisho la Mpira wa barani Afrika (CAF), limevipitisha Viwanja vya Uhuru, Dar es Salaam na CCM Kirumba, jijini Mwanza kwa ajili ya michuano mbalimbali ya kimataifa ngazi ya klabu na timu za taifa.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linachukua nafasi hii kuwapongeza wamiliki viwanja hivyo kwa namna walivyoweza kutunza hadi kukidhi matakwa ya CAF.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni