Manchester City imezidi kuimarisha
matumaini yake ya kumaliza katika nafasi nne za juu za Ligi Kuu ya
Uingereza kwa kupata ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Southampton.
Beki anayekabiliwa na majeruhi
Vincent Kompany alifunga goli la kwanza katika kipindi cha pili kwa
kichwa akiunganisha mpira wa krosi ya winga wa kushoto David Silva.
Leroy Sane aliongeza la pili
akiunganisha kwa shuti pasi ya Kevin de Bruyne katika shambulizi la
haraka na kisha Sergio Aguero akafunga la tatu.
Beki Vincent Kompany akifunga kwa kichwa goli la kwanza katika mchezo huo
Dogo Mjerumani Leroy Sane akiifungia Man City goli la pili
Katika mchezo mwingine Tottenham
imekwea hadi pointi nne nyuma ya vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza
Chelsea baada ya kupata ushindi wa magoli 4-0 Bournemouth.
Katika mchezo huo Mousa Dembele
aliifungia Spurs goli la kwanza, Son Heung-min akaongeza goli la pili
na Harry Kane akafunga la tatu kisha Vincent Janssen akafunga la nne.
Son Heung-min akifunga goli la pili la Tottenham
Harry Kane akifunga goli la tatu la Tottenhm
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni