Uongozi wa Chelsea katika Ligi Kuu
ya Uingereza umepunguzwa na kuwa tofauti ya pointi nne, baada ya jana
kukubali kipigo cha magoli 2-0 kutoka kwa Manchester United katika
dimba la Old Trafford.
Kocha wa United, Jose Mourinho
alikuwa amefungwa magoli 4-0 katika mchezo wao wa kwanza wa ligi na
Chlesea pia alitolewa na timu hiyo aliyowahi kuinoa katika mchezo wa
robo fainali ya FA katika dimba la Stamford Bridge.
Safari hii Mourinho alirekebisha
makosa huku akiwatumia washambuliaji Marcus Rashford na Jesse Lingard
akimpumzisha Zlatan Ibrahimovic na mbinu hiyo ilizaa matunda pale
Rashford alipofunga goli la kwanza dakika ya 7 na kisha Ander Herrera
kufunga la pili.
Marcus Rashford akifunga goli la kwanza katika dakika ya saba tu ya mchezo
Mpira uliopingwa na Ander Herrera ukimshinda kipa wa Chelsea na kujaa wavuni
Kiungo Paul Pogba akimdhibiti mshambuliaji Diego Costa asilete madhara
Katika mchezo mwingine Roberto
Firmino amefunga goli lililoipa ushindi Liverpool kwa mara ya pili
ndani ya wiki mbili wakati wakiibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya
West Brom.
Roberto Firmino akifunga kwa kichwa goli pekee la Liverpool katika mchezo huo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni