Na Mwandishi Wetu
BENKI ya NMB imeshiriki kampeni zilizoendeshwa na Shirika la Kimataifa la Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo UN- CDF zinazowakutanisha vijana pamoja na mashirika mbalimbali yanayofanya kazi kuwahusisha maendeleo ya vijana. Kampeni hizo 'BankTheYouth' zilizowakutanisha vijana na kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili zimelenga kuhamasisha vijana nchini kupata uelewa wa masuala ya fedha pamoja na kuwaunganisha na taasisi zinazowainua vijana kimitaji ili wafikie malengo yao.
Akizungumza na vijana walioshiriki kampeni hizo, Meneja Mwandamizi Kitengo cha Amana, Bima na Huduma za ziada wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Adili alisema vijana wanapaswa kuungana katika vikundi na kuandaa maandiko ya biashara ambayo yataivutia benki kutoa mikopo ili kuendesha biashara zao. Alisema benki ya NMB imekuwa mstari wa bele kuibua bidhaa mbalimbali za kibenki zinazolenga kuwainua vijana hasa elimu ya uelewa masuala ya fedha na namna ya kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba.
Aliwashauri vijana kutembelea matawi mbalimbali ya NMB na kujenga urafiki kwa kufungua akaunti na kujiwekea akiba kabla ya kuanza kunufaika na bidhaa mbalimbali zilizoanzishwa kuwasaidia vijana kimitaji. "...Ili benki ikuamini lazima ujenge mahusiano mazuri, ujenge urafiki na hii ni pamoja na kuwa na akaunti na sisi. Hatuwezi kukuamini kama hata hauna akaunti na sisi, anza kwa kujenga mahusiano mazuri kwanza nasi ndipo tukuamini...hatuwezi kukukopesha kama haupo karibu na sisi," alisema Adili.
Kwa upande wake Mkurungenzi Mkuu wa UN CDF Tanzania, Peter Malika aliwataka vijana kushiriki vema katika kampeni hizo pamoja na kukubali kubadilika kulingana na mazingira ya sasa na kutumia fursa zilizopo ili ziwaletee maendeleo. Aliwataka kujadiliana na kuibua changamoto anuai ambazo zimekuwa vikwazo katika maendeleo yao.
Alisema lazima wajiweke katika vikundi na kufuata utaratibu mzuri utakaowekwa na taasisi zinazosaidia vijana kuelekea katika maendeleo. Aidha aliongeza kuwa vikundi vya vijana lazima vijulikane na kufuata utaratibu rasmi uliowekwa ili viweze kuaminika kwa taasisi mbalimbali zikiwemo za kifedha. Aliwaomba wajiwekee utaratibu wa kujiwekea akiba ili waweze kuaminika zaidi.
Naye Ofisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Maendeleo ya Vijana, Eliakimu Mtawa aliwataka vijana kujenga uaminifu wa kurejesha mikopo pale wanapopata fursa ya kukopeshwa kwani takwimu zinaonesha fedha nyingi zinazotolewa na Serikali kuwakopesha vijana wapate mitaji wamekuwa hawarejeshi jambo ambalo linatishia uhai wa mifuko hiyo kuendelea kusaidia vijana wengine.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni