.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 4 Aprili 2017

RAIS WA ZANZIBAT DKT SHEIN AKIWA ZIARANI MKOA WA KASKAZINI PEMBA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Crispin Prospher Mwombeki wa kampuni ya Ujenzi wa Barabara ya Mecco wakati Rais alipotembelea ukarabati wa barabara ya Chwale (Madenjani) mpaka Mzambarautakao inayojengwa na kampuni hiyo yenye urefu wa kilomita tano (5km) katika Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba leo akiwa katika ziara ya kikazi (kulia) katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Miundombinu Nd,Mustafa Aboud Jumbe
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Miundombinu Nd,Mustafa Aboud Jumbe (kulia) wakati alipotembelea ukarabati wa ujenzi w Barabara ya Chwale (Madenjani) mpaka Mzaambarautakao leo inayojengwa na kampuni ya Ujenzi wa Barabara ya Mecco yenye urefu wa kilomita tano (5km) katika Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba akiwa katika ziara ya kikazi (kulia)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto)akipata maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Miundombinu Nd,Mustafa Aboud Jumbe (katikati) alipokuwa akiangalia mashine ya kutilia lami (PAVER) ya kampuni ya Mecco leo wakati alipotembelea ukarabati wa ujenzi wa Barabara ya Chwale (Madenjani) mpaka Mzambarautakao inayojengwa na Kampuni hiyo yenye urefu wa kilomita tano (5km) katika Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, akiwa katika ziara ya kikazi (kulia)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(katikati)akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya ZECON ya Zanzibar Nd,Ali Mbarouk Juma (kulia) wakati alipofika Daya Mtambwe Kaskazini Pemba kuangalia hatua za Ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali leo akiwa katika ziara ya kikazi Mkoa wa Kasakazini Pemba,(wa pili kulia)Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Mmanga Mjengo Mjawiri
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akizungumza na Wananfunzi wa Skuli ya Daya Mtambwe leo alipotembelea Ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali unaojengwa na Kampuni ya kizalendo ya ZECON ya hapa Zanzibar, akiwa katika ziara ya kikazi Mkoa wa Kasakazini Pemba
Wanafunzi wa Skuli ya Msingi ya Daya Mtambwe wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati alipofika Skulini hapo leo kuangaalia ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali unaojengwa na Kampuni ya kizalendo ya ZECON ya hapa Zanzibar akiwa katika ziara ya kikazi Mkoa wa Kasakazini Pemba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(katikati)akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Rashid Hadid Rashid alipotembelea Ukunjwi katika sehemu ya kupokelewa Umeme unaopelekwa kisiwa cha Fundo, Mkoa wa kaskazini Pemba akiwa katika ziara ya kikazi leo [Picha na Ikulu.]03/04/2017.

Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ametembelea miradi ya maendeleo kisiwani Pemba ukiwemo mradi wa barabara, umeme na Chuo cha Mafunzo ya Amali na kuitaka Kampuni ya ZECON inayojenga Chuo hicho kuhakikisha mradi wa ujenzi huo unakamilika kwa muda uliopangwa.

Akiwa katika eneo la chuo hicho huko Daya Mtambwe mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa Kampuni ya Ujenzi pamoja na Mshauri Mwelekezi alisisitiza kuwa mradi huo ni wa Serikali na Wizara ya Elimu ni wasimamizi tu, hivyo alieleza umuhimu wa kumalizika mapema mradi huo kwa maslahi ya wananchi.

Alieleza kuwa changamoto za kiufundi zilizojitokeza katika kutekeleza mradi huo hazina budi kupatiwa ufumbuzi wa haraka ili utekelezaji wa mradi huo uweze kukamilika kama ilivyopangwa.

Mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa Chuo cha Amali kilichopo Daya Mtambwe, Dk. Shein alipata nafasi ya kuzungumza na wananchi pamoja na wanafunzi wa Skuli ya Msingi Daya katika viwanja vya skuli hiyo na kusisitiza lengo la Serikali la kujenga chuo hicho.

Dk. Shein alisema kuwa ujenzi wa Chuo hicho utawasaidia wale wanafunzi waliokuwa hawakupata fursa ya kuendelea na masomo ya juu na kuweza kupata mafunzo ya vitendo yakiwemo mafunzo ya kiufundi.

Alisema kuwa uwamuzi wa Serikali ni kujenga chuo hicho kama kilivyo chuo cha Amali cha Vitongoji kwa upande wa Pemba na Mkokotoni Unguja na kusisitiza kuwa ujenzi huo utakwenda sambamba na ujenzi wa chuo cha Amali huko Makunduchi.

Aidha, Dk. Shein alisema kuwa ujenzi wa Chuo hicho ni ahadi aliyoitoa wakati wa Kampeni za uchaguzi mkuu uliopita wakati akiwahutubia wananchi huko Kangagani, na kusisitiza utekelezaji wa ahadi yake hiyo upo pale pale.

Alisema kuwa licha ya ujenzi huo kusita kutokana na sababu za kiufundi kwa takriban miezi saba kwa hivi sasa na kueleza kuwa si zaidi ya wiki tatu ujenzi huo utaendelea na matarajio ni kumalizika hapo mwakani.

Mapema Dk. Shein alipata fursa ya kukagua ukarabati wa barabara ya Chwale (Madenjani) hadi Mzambarautakao wenye urefu wa kilomita 5 unaoendelea kwa kiwango cha lami ambao unatarajiwa kumalizika baada ya wiki moja.
Mkuu wa Mradi kutoka Kampuni ya MECCO, Crispin Prosper Mwombeki, alimueleza Dk. Shein kuwa ukarabati huo baada ya miezi saba umefanywa kwa muda wa miezi mitatu ili kwenda na hali halisi ya jiografia ya Pemba.

Pamoja na hayo, Mwombeki alieleza changamoto zilizopo hasa katika suala zima la utaratibu wa upatikanaji wa kifusi kwa ujenzi wa barabara huku akieleza haja ya kuweko na utaratibu wa kudumu wa ukarabati wa barabara hizo ndani ya mwaka mmoja.

Wakati huo huo, Dk. Shein alifika Ukunjwi kwa ajili ya kuangalia mradi wa umeme unaopelekwa katika kisiwa cha Fundo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni