.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 31 Mei 2017

KAMPUNI YA EVERGREEN LIMITEDE YATOA MSAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO VISIWANI ZANZIBAR

Meneja wa Kampuni ya Hawaii Clearing and Fowarding Bwana Thabit Maalim Kulia akimkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Paketi za Mchele Tani Moja na Nusu kwa ajili ya Wananchi walioathirika na Mvua za Masika.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kulia akipokea Saruji Paket 1,000 kutoka kwa Meneja Mkuu wa Kampuni ya Evergreen Limited Bwana Abdughafur Ismail kwa ajili ya Wananchi walioathirika na Mvua za Masika hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Balozi Seif akiyashukuru Makampuni yaliyojitokeza kusaidia Waathirika wa Mavua za Masika baada ya kupokea Msaada wa Mchele na Saruji kutoka kwa Kampuni ya Evergreen Limited na Hawaii Clearing and Fowarding.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akisalimiana na Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar {SUZA} kutoka Nchini Cuba hapo kwenye makaai yao Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
 Aliyempa Mkono ni Dr. Luis Alfonso, wa kwanza kutoka Kulia ni Dr. Dr. Maria Del Carmen na kulia ya Dr. Alfonso ni Dr. Rosario Maria Acosta.
Balozi Seif Kulia akibadilishana mawazo na Wahadhiri wa Suza kutoka Nchini Cuba.

Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar {SUZA} kutoka Nchini Cuba wakiwa makini kufuatilia mazungumzo ya Balozi Seif hapo kwenye makaazi ya Mbweni
Mkuu wa Timu ya Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha SUZA kutoka Cuba Dr. Luis Alfonso akiwasilisha salamu zao za shukrani kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Seif.


                                                                                                 Picha na – OMPR – ZNZ.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepokea msaada wa Paketi 1,000 za Saruji kutoka kwa Kampuni ya Evergreen Limited na Tani moja na nusu za mchele kutoka kwa Kampuni ya Hawaii Clearing and Forwading kwa ajili ya kusaidia Wananchi waliopatwa na maafa ya mafuriko ya Mavua za Masika zinazokaribia ukiongoni mwake.

Msaada huo umepokelewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi seif Ali Iddi ulioshuhudiwa pia na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed na maafisa watendaji wa Ofisi hiyo hapo Vuga Mjini Zanzibar.

Bwana Abdulghafar Ismail Meneja Mkuu wa Kampuni ya Evergreen Lilited alikabidhi saruji hiyo kwa niaba ya Kampuni yenye thamani ya shilingi Milioni 14,000,000/- na Bwana Thabit Maalim Meneja wa Kampuni ya Hawaii Clearing and Fowarding akakabidhi msaada wa mchele kwa niaba ya Taassi yake wenye Thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni Moja na Nusu.

Wawakilishi hao wa Kampuni hizo za Kibiashara Zanzibar walisema wameamua kutoa misaada hiyo wakiitikia wito wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa kuwataka Wananchi, Wafanyabiashara na Wahisani kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuwasaidia Wananchi waliokumbwa na Maafa ya mvua za Masika.

Walisema maafa waliyoyapata Wananchi hao katika maeneo mbali mbali ya Visiwa vya Unguja na Pemba yameleta fadhaa na kuwafanya kukosa muelekeo wa kuanza upya kwa harakati zao za kimaisha kiasi kwamba hali hiyo wanastahiki kupata msukumo utakaowapa matmaini mapya.

Akipokea msaada huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliushukuru Uongozi wa Kampuni ya Evergreen Limited na ule wa Hawaii Clearing and Fowarding kwa imani ulioonyesha wa kusaidia waathirika wa Mafuriko ya Mvua za Masika.

Balozi Seif alisema Wananchi wote waliokumbwa na mafuriko hayo katika maeneo tofauti Unguja na Pemba wanastahiki kupata msaada na wale walioguswa na tukio hilo wanapaswa kuwaonea huruma waathirika hao.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwahakikishia Viongozi wa Kampuni hizo kwamba msaada waliotoa utawafikia walengwa katika kipindi kifupi ili uwasaidiae kuondokana na shida zinazowakabili kipindi hichi kugumu.

Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewatembelea Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar {SUZAZ} kutoka Nchini Cuba hapo kwenye Makaazi yao Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Balozi Seif amewaahidi Wahadhiri hao kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini mchango unaotolewa na Serikali ya Cuba hasa katika Sekta ya Afya na Elimu kwa kuleta Wahadhiri wanaofundisha Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar {SUZA}.

Aliwahakikishia Wahadhiri hao wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar {SUZA} kutoka Nchini Cuba kuishi kwa Amani na Serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi itazingatia maisha yao bila ya wasi wasi wowote.

Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ikifanya jitihada za kutafuta wataalamu wa Kigeni kusaidia fani tofauti za ujuzi Nchini ili kuwapa faraja wananchi wake kuweza kukabiliana na harakati zao za kimaisha za kila siku.

Naye Mkuu wa Timu ya Wahadhiri hao wa Cuba Dr. Luis Alfonso kwa niaba ya Wahadhiri wenzake ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuvishukuru vyombo vya ulinzi kwa hatua za haraka zilizochukuliwa katika kuwapa ulinzi wa uhakika Wahadhiri hao.

Timu ya Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar { SUZA } kutoka Nchini Cuba wameanza kusomesha Chuo hicho kwa utaratibu wa Miaka Mitatu.

Othman Khamis Ame

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar












Hakuna maoni :

Chapisha Maoni