Msemaji wa rais Robert Mugabe wa
Zimbabwe amesema rais huyo huwa halali katika mikutano kama
inavyodaiwa bali hufumba macho yake kwa muda mrefu ilikuyapumzisha.
Msemaji huyo George Charamba amesema
rais Mugabe hufumba macho kuyaepusha na mwanga.
Imekuwa kawaida sasa
kwa rais Mugabe kulala kwenye matukio kadhaa na kuibua hofu ya hali ya afya yake.
Rais Mugabe hivi karibuni amekuwa
akipatiwa matibabu maalum ya macho nchini Singapore.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni