Manchester United imetwaa kumbe la
pili kubwa katika msimu huu na kufanikiwa kutinga katika Ligi ya
Mabingwa Ulaya baada ya kuifunga Ajax magoli 2-0 na kushinda Ligi ya
Uropa Jijini Stockholm.
Katika usiku uliojawa huzuni
kufuatia shambulizi lililouwa watu 22 katika tamasha la mwanamuziki
Ariana Grande katika ukumbi wa Manchester Arena jumatatu mashabiki wa
Manchester United walilazimika kutoshangilia kupitiliza.
Manchester United ilipata goli la
kwanza kupitia shuti la Paul Pogba lililogongwa na kumpoteza uelekeo
goli kipa katika dakika ya 18 na kisha baadaye Henrikh Mkhitaryan
akafunga goli lake la sita katika michuano hiyo akiunganisha mpira wa
kona uliopigwa kichwa na Chris Smalling.
Mpira uliopigwa na Paul Pogba ukimshinda kipa wa Ajax na kujaa wavuni
Henrikh Mkhitaryan akiangalia mpira alioupiga ukielekea kujaa wavuni
Kocha Jose Mourinho akinyanyuliwa juu na timu yake ya ufundi baada ya ushindi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni