Mradi
huo mkubwa wa maji umetumia takribani milioni 200 ikiwa ni gharama
nzima za mradi huo, utekelezaji wa mradi huo umesimamiwa na mamlaka ya
hifadhi ya Ngorongoro ikiwa ni utekelezaji wa agizo la waziri mkuu Mhe.
Kassim Majaliwa alilolitoa mapema mwezi wa Desemba 2016, moja ya maagizo
yake ilikua ni wananchi kujengewa mfumo wa maji kwa matumizi yao na
mifugo yao ili kuzuia uingizwaji wa mifugo katika crater ya Ngorongoro.
Aidha
Mhe. Gambo ameipongeza mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kwa kuutekeleza
mradi huo kwa wakati na kuendelea kutoa msisitizo kwa wananchi kuwa
agizo la kutoingiza mifugo ndani ya crater linaendelea na amezitaka
mamlaka kuanza mchakato wa kuligeuza agizo hilo kuwa sheria ili liweze
kutekelezeka kwa vitendo zaidi.
Wananchi
wa eneo la Ndepes wameishukuru sana serikali ya awamu ya tano kwa
kutekeleza ahadi yake ya kuhakikisha wananchi hawafuati maji umbali
zaidi ya mita mia nne kama ilivyo ahidiwa katika ilani ya Chama Cha
Mapinduzi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni