.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 24 Mei 2017

PHIRI:MSIMU MBAYA NA MATOKEO YA KUSHANGAZA – MBEYA CITY

JUMAMOSI Mei 20, kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea, Mbeya City fc ilicheza mchezo wake wa mwisho wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2016/17 na kupoteza kwa bao 2-1 dhidi ya wenyeji Majimaji Fc waliocheza mchezo huo wakiwa na presha kubwa ya kuepuka kushuka daraja jambo lililowachagiza kucheza kwa nguvu zote na hatimaye kufanikiwa kusalia kwenye ligi kufuatia ushindi huo.

Katika mahojiano maalumu na mbeyacityfc.com kocha mkuu Kinnah Phiri alisema City imekuwa na msimu mbaya wenye matokeo ya kushangaza licha ya kuanza vizuri kwa ushindi wa michezo miwili na sare moja kwenye michezo mitatu ya mwanzo wa msimu huko kanda ya ziwa matokeo yaliyoipa nafasi ya kuongoza ligi kwa mara ya kwanza tangu kupanda daraja 2013/14.

Tulianza msimu vizuri,kikosini kila mmoja alikuwa na ari kubwa baada ya michezo ya kanda ya ziwa tulirudi nyumbani kucheza na Prisons,baada ya hapo tuliingia kwenye wakati mgumu,hatukuwa vizuri tena,tulifanya kila lililowezekana lakini haikuweza kuwa sawa,mambo kadhaa yalijitokeza,uwepo wa vijana wengi wapya ilikuwa mojawapo ya mambo hayo, kuna wakati ilituwia vigumu kuwaunganisha ili wacheze kama timu kwa sababu mbalimbali.


Mwisho wa siku naweza kusema umekuwa msimu mbaya wenye matokeo ya kushangaza kwa sababu hata michezo ambayo tulicheza kwa kiwango cha juu ajabu baada ya dakika 90 sisi ndiyo tulipoteza mchezo,hivyo naweza kuongeza kuwa tumepita kwenye wakati mgumu wa ujenzi wa kikosi chetu kumbukumbu zinaonyesha tuliingiza wachezaji wengi dirisha dogo nadhani inahitaji muda kuwafanya wawe kitu kimoja imani yangu kubwa tutakuwa tayari zaidi msimu ujao.

Akiendelea zaidi Phiri alisema kuwa katika dakika zote 2,700 ambazo City imeshuka uwanjani msimu huu imefanikiwa kufunga mabao 27 pekee huku ikiruhusu mabao 32 jambo linaloonyesha kuwa hakukuwa na uwiano mzuri kikosini kwenye safu za ulinzi na ushambuliaji, uhai pekee ulikuwa kwenye safu ya kiungo ambayo pia ndiyo imetoa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi ya wote.

Hii ni tofauti kubwa na msimu uliopita ambao tulifunga mabao 32 na kufungwa 34, safu ya kiungo imetoa mchezaji aliyefunga mabao mengi ya msimu hii ni tafsiri kuwa tunahitaji kuimarisha zaidi sehemu za ushambuliaji na ulinzi, ili tuweze kufunga mabao mengi pia kujilinda vyema,hili tutalifanya msimu ujao kwa sababu tumelingundua na sasa ndiyo mikakati yetu katika kutafuta ubingwa wetu wa kwanza,ni wazi maeneo hayo yatakuwa kipaumbele katika usajili tutakao ufanya.

Tukifanikiwa hilo ni wazi msimu ujao utakuwa mzuri,City ni moja ya timu nzuri katika ligi,mbinu na mifumo ambayo tumejifunza msimu huu nadhani itakuwa imekomaa vizuri kwa vijana,tutarekebisha machache yaliyosalia kuifanya timu kuwa bora zaidi, utakuwa msimu wa tano katika ligi jambo muhimu kwetu wakati huo litaakuwa ni kugombea ubingwa na si vingenenyo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni