Mkoa wa Cape ya Magharibi ya Afrika
Kusini, umetangaza kukabiliwa na janga la ukame wakati ukikabiliwa na
uhaba mkubwa wa maji kuwahi kutokea tangu miaka 113 kupita.
Mkuu wa Mkoa huo, Helen Zille,
amesema watalazimika kuchimba visima kwa ajili ya kupata maji ya
kutumika katika maeneo muhimu ya mji wa Cape zikiwemo hospitali.
Tahadhari hiyo itadumu kwa miezi
mitatu, lakini inaweza kuongezwa muda iwapo ukame utaendelea.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni