Na Dotto Mwaibale, Mwanza
WAANDISHI wa Habari wanaounda Chama cha Waandishi wa Habari za Kilimo wamekutana Malaika Beach Resort jijini Mwanza kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali ya chama hicho.
Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika jana Mwenyekiti wa chama hicho, Gerald Kitabu pamoja na mambo mengine alihimiza wanachama ambao bado hawajatoa michango yao ya mwaka waitoe ili kutunisha mfuko wa chama hicho.
“Ni muhimu wanachama ambao bado hawajaotoa michango yao kuhakikisha wanaitoa kwa wakati” alisema Kitabu.
Katibu wa Chama hicho, Elias Msuya alisema chama hicho kipo katika mchakato wa kutengeneza vitambulisho kwa ajili ya wanachama na wakati wowote vitakapo kuwa tayari vitatolewa kwa wahusika.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni