Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo, Dk. Harrison George Mwakyembe leo Jumatano Mei 24, 2017
ataongoza viongozi na wanafamilia wengine wa michezo hususani mpira
wa miguu kuilakini Serengeti Boys - timu ya soka ya Tanzania ya
Vijana wenye umri wa miaka 17.
Serengeti Boys inatarajiwa kutua
Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam,
Tanzania leo saa 8:50 mchana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Afrika
Kusini ikitokea Libreville, Gabon kupitia Johannesburg nchini Afrika
Kusini.
Mara baada ya kutua, timu itakwenda
Hoteli ya Urban Rose kupata mapumziko angalau ya siku moja kabla ya
TFF kuandaa utaratibu wa kuagana nao.
Baada ya Mheshimiwa Waziri Dk.
Mwakyembe kuthibitisha kutokea Uwanja wa Julius Nyerere kuilaki timu,
Rais wa TFF, Jamal Malinzi amesema: “Tunamshuru sana Mheshimiwa
Waziri kwa kuwapokea vijana ambao sasa wanaunda kikosi kipya cha
taifa cha vijana wenye umri wa chini ya miaka 20.
“Kauli mbiu yao - ‘Ngorongoro
Heroes kunyaga twende mpaka kufuzu fainali za AFCON u 20 mwaka 2019’,
michezo ya kufuzu kwa hatua hiyo ya fainali za U-20 zitaanza Aprili,
mwakani. Vijana hawa wataingia kambini tena mwezi Oktoba, mwaka huu
na watacheza mechi ya kimataifa ya kujipima nguvu.
“Mpira huwa haulali, unachezwa saa
24 katika wiki duniani ambako huanzia Januari hadi Desemba,
likimalizika shindano hili linakuja jingine. Maumivu ya kufungwa huwa
ni mafupi, mashabiki siku zote huwa wanafkiria mechi ijayo. Tujiandae
na Qulifiers za 2019 AFCON u-20, haziko mbali.” amesema.
Timu hiyo ya vijana ilikuwa jijini
Libreville nchini Gabon kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya
Afrika ya vijana iliyofanyika katika miji miwili ya Libreville na
Port Gentil ambako iliondolewa kwenye hatua ya makundi na Niger.
Serengeti Boys ilifungwa bao 1-0 na
Niger katika mchezo uliofanyika Port Gentil, hivyo kufanya matokeo ya
timu zote mbili yaani Niger na Tanzania kufanana kwa pointi, idadi ya
mabao ya kufunga na kufungwa tangu kuanza kwa fainali hizi za AFCON,
Mei 15, mwaka huu.
Serengeti Boys iliyokuwa Kundi B
iliondolewa Kundi B iliondolewa na Niger iliyopenya kwenda hatua ya
Nusu Fainali kwa faida ya kupata ushindi katika mchezo ambao
umekutanisha timu hizo kwani Tanzania ilifungwa 1-0 katika mchezo wa
mwisho hatua ya makundi.
Kanuni hiyo ya mashindano ya CAF
inajieleza kuwa matokeo ya ‘head to head’ kwa maana zinapokutana
timu mbili zenye uwiano wa pointi na magoli matokeo huamualiwa kwa
mshindi kupewa nafsi katika mchezo uliokutanisha timu hizo mbili.
……………………………………………………………………..……………..……
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA
MIGUU TANZANIA
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni