![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgxJUi-meEVqFQzmVIMsRjmATqD9INZns7UZKwjLbgYD0VkUTjI_EbiIrnGGZ1eeq9lbNrhePjK5-dshNsJzXQ7XJ7p25v_Ur32jF9ouYPtUrmug8eD6uKbqe1kQzlSXDCzGIL_C01t8tVA/s640/812.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi8K76negMEpZd3Rnt1lFUEHNDF0X38eBevtIK1gkGTP6JNZvSTQI-SXhErKCO0Q2jch5-hkcZyQF5ytRLrZuZXAf-5Jn1FjV8itn8VFEvQ6wUQNwzeNl-zGdxxyY4_W4ifBCfg4Yjedd8y/s640/821.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi6c3sIle6zX2Sw6IPpbu5FdxCo_G7sII03qMQY-8rgqYy1341mAO9cPiMJLA0jEgPgepiPiwVow6gwicHeXBtXOyNkqVLH7MoGXethyNlneNd1HRsmtQafNmRIRp8iXcmNbzrs2eNB20c-/s640/828.jpg)
Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini Tanzania {TFF }limepeleka maombi kwenye Shirikisho la Soka Duniani { FIFA } kuiomea Zanzibar kuwa Mwanachama wa Shorikisho hilo.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Muandamizi anayeshughulikia ruzuku wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania {TFF} Derek Murusuri wakati akiwasilisha salamu za Rais wa Shirikisho hilo Jamal Malinzi kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Baraza la Wawakilishi Mbweni.
Derek Murusuri alisema Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania limeshaiandikia Barua rasmi FIFA kuhusu suala hilo lilalosubiriwa na wapenda soka wa Visiwa vya Zanzibar kuwa na uweo wa kushiriki moja kwa moja michezo ya Kimataifa inayoandaliwa na Shirikisho hilo la Dunia.
Alisema mipango inaandaliwa na Uongozi wa juu wa TFF katika kuhakikisha inaipatia nakala Zanzibar kuthibitisha hatua zilizokwishachukuliwa na Uongozi huo wa juu wa Soka Tanzania.
Afisa Muandamizi huyo anayeshughulikia ruzuku wa TFF alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba TFF hivi sasa inaendelea na mikakati ya kukusanya Vijana wenye vipaji kwa lengo la kuwandaa kupitia mashindano mbali mbali ya Kitaifa na Kikanda kwa kuwaona ili kupata Timu imara itakayokuwa na uwezo wa kushiriki Kombe la Dunia mwaka 2026.
Aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Taasisi zake zinazosimamia michezo pamoja na washirika wa Sekta hiyo kwa juhudi ilizochukuwa za kuisaidia Timu ya Taifa ya Viwanja wenye umri wa chini ya miaka 17 ya Serengeti Boys.
Alisema Timu hiyo kwa kiasi kikubwa imeweza kuipa heshima kubwa Tanzania kwa kiwango ilichofikia katika mashindano ya hivi karibuni ya kuwania Kombe la Dunia linalotarajiwa kufanyika India kwa kutolewa na Timu ya Soka ya Niger katika hatua ya Robo Fainali.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliupongeza Uongozi mzima wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania kwa hatua uliofikia wa kuisimamia Zanzibar katika maombi hayo.
Balozi Seif alisema Zanzibar imekuwa katika harakati za kutafuta fursa ya kuwa mwanachama wa Shirikisho la Mpira wa Soka Duniani FIFA kwa kipindi kirefu sasa licha ya vikwazo na changamoto nyingi zilizojitokeza na kukwaza ucheleweshaji huo.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni