Timu ya Manchester United inajipanga
kunasa saini ya winga wa Inter Milan, Ivan Perisic, kwa ada ya
uhamisho wa kitita cha puandi milioni 44.
Kocha Jose Mourinho anaimani na
winga huyo wa Inter Milan, mwenye miaka 28, kuwa atakuwa muhimili
muhimu katika kuimarisha kikosi chake kwa Ligi Kuu ya Uingereza.
Hakuna kiasi cha fedha
kilichokubaliwa hadi sasa, lakini mazungumzo ya awali yamefanywa na
klabu hizo, na Mourinho anamtaka mchezaji huyo katika maandalizi ya
msimu mpya.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni