Na Shushu Joel,MAGU.
MASHINDANO ya urembo ngazi ya wilaya yanayojulikana kwa la jina Miss Mazingira yameanza kupamba moto kwa washiriki ambao wako kambini kujitokeza kushiriki kazi mbalimbali za kijamii katika maeneo tofauti tofauti ya wilaya ya Magu mkoani Mwanza.
Wakizungumza wakati wa kufanya usafi katika hospital ya wilaya, washiriki hao walisema kuwa lengo la shindano hilo ni kuwafumbua macho watanzania hasa wakazi wa Magu kuweza kubadilika kimawazo ili kila mmoja ajione ni jukumu lake kufanya usafi wa mazingira na si kuachia serikali tu katika usafi wa mazingira yetu.
Susana Peter ni mmoja wa washiriki wa kuwania taji la Miss Mazingira ambaye pia ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Magu day anasema kuwa lengo lake ni kushinda taji hilo na kuhamasisha jamii kuweza kutambua umuhimu wa kutunza mazingira ili eneo letu liweze kupendeza na hata kuvutia kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Aliongeza kuwa lengo lake si kupata taji, bali kuibadilisha jamii iliyojaa kila aina ya lawama kwa serikali juu ya uchafu unaozagaa kila kona ya eneo la Magu.
“Jamii sasa inatakiwa kubadilika na kufanya kazi kwa mazoea kama walivyokuwa wakifanya miaka ya nyuma kwa kuacha mazingira yakiwa katika hali ya kuvutia na hata kufanya upatikanaji wa asali nyingi kwa kuwa nyuki walikuwepo lakini kwa sasa ni tofauti nah ii ni kutokana na uchafuzi wa mazingira ikiwemo ukataji wa miti ovyo”
Aidha ameitaka jamii kuweza kutunza mazingira kuanzia majumbani kwao ndio mfano mzuri na ni wa kuigwa na watu mbalimbali pale mfano unapokuwa wewe mwenyewe binafi na si kutoa hamasa tu huku wewe ukiwa na ziro.
Kwa upande wake Mery Julius ambaye ni mshiriki wa mashindano hayo anasononeshwa na kitendo cha serikali kutoyakazia mashindano ya u Miss kwa kigezo cha kuwa labda ni uhuni kama wengi wanavyofikilia.
Aliongeza kuwa ukitunza mazingira utakuwa na faida nyingi katika jamii ikiwemo kupata watalii ambao wanapenda kuja kutembelea na kujionea uoto wa aina mbalimbali lakini kwa sasa imekuwa wakienda mbungani tu kuona wanyama si kama ilivyokuwa zamani hata kuona mazingira mengine kama ya miti ya asili.
Olivian Mganga ni mwandaaji wa mashindano hayo anadai kuwa lengo la mashindano hayo ni kupambana na uchafu wa mazingira unaozidi kujitokeza siku hadi siku katika jamii yetu na ndio sababu iliyomfanya kuanzisha kwa mashindano hayo kwa lengo la kupata mtu atakaye kuwa mstali wa mbele katika umamasishaji wa utunzaji wa mazingira katika Nyanja mbalimbali.
Mganga aliongeza kuwa katika hali ya sasa kuna changamoto nyingi zinazojitokeza katika ufanikishaji wa mashindano hayo kubwa ni wazazi wengi kutowaruhusi mabinti zao kushiriki kutokana na imani potofu kuwa u miss ni uhuni.
Aliongeza kuwa changamoto nyingine kukosekana kwa wafadhili wa mashindano hayo hivyo kila kitu ni yeye mwenyewe na huku yeye aliyaanzisha kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa jinsi yalivyo hivi sasa kwani maeneo mengi yamekuwa ni majangwa na hii ni kutokana na watu kukata miti ovyo na utunzaji mbaya wa mazingira,naomba watu waweze kujitokeza ili kufanuikisha mashindano hayo.
Aidha aliongeza kuwa washiriki wote watapata zawadi ila washindi watatu wa juu watakuwa na zawadi kubwa zaidi na ili ni kutokana na washiriki kuwa wengi kuliko tulivyotarajia,washiriki wapo 25 na mshindi wetu atapatikana siku ya tarehe 1 ya mwezi wa saba na katika sherehe hizi mgeni rasmi ni mkuu wetu wa wilaya Bi,Khadija Nyembo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni