Mama mmoja huko Texas Marekani
anakabiliwa na mashtaka ya kusababisha vifo vya watoto wake wawili
kwa joto baada ya kuwafungia kwenye gari lililoegeshwa juani mwezi
uliopita.
Polisi nchini Marekani wamesema mama
huyo Cynthia Marie Randolph amesema alikuwa amefanya kitendo hicho
ili kumtia adabu mtoto wake wa kike wa miaka miwili aitwaye Juliet
baada ya kukataa kutoka kwenye gari.
Mtoto Juliet pamoja na mdogo wake wa
kiume wa miezi 16 Cavanaugh walithibitishwa kufa kwa joto na kukosa
hewa Mei 26 majira ya saa kumi na nusu jioni, wakiwa kwenye joto la
nyuzi joto 35.5.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni