Nyota wa mpira wa tenesi Venus
Williams amehusika katika tukio la ajali ya gari iliyosababisha kifo
cha mzee wa miaka 78.
Msemaji wa Kituo cha Polisi cha Palm
Beach Gardens huko Florida amethibitisha kuwa wanafanya uchunguzi wa
ajali hiyo mbaya inayohusiana na bingwa huyo wa Grand Slam.
Mwanaume aliyegongwa na gari hilo
alikimbizwa hospitali Juni 9, na alifariki dunia wiki mbili baadaye
kutokana na majeraha aliyoyapata.
Kwa mujibu wa TMZ, walioibua habari
hiyo, polisi wanaamini lilikuwa ni kosa la Venus lakini mwanasheria
wake anasema ilikuwa ni ajali tu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni