.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 25 Juni 2017

MCHEZAJI MAMADOU SAKHO WA LIVERPOOL ATEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA SOS ZANZIBAR

Mchezaji wa Timu ya Liverpool Mamadou Sakho akisalimiana na Watoto wa Kijiji cha Watoto SOS mombasa Zanzibar alipowasili katika kijiji hicho kuwatembelea watoto hao na kukabidhi vyakula kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Eid el Fitry wiki ijayo kuweza kujumuika na watoto wenzao kufurahiyi sikukuu hiyo baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Watoto wa Kijiji cha SOS Zanzibar wakiwa na mabango ya kumkaribisha Mchezaji wa Timu ya Liverpool Mamadou Sakho katika viwanja vya Kijiji chao mombasa Zanzibar kuwatembelea na kukabidhi msaada wa Vyakula kwa Watoto hao akiwa na Mke na Watoto wake.
Mchezaji wa Timu ya Liverpool Mamadou Sakho akiwa katika picha ya pamoja na Watoto wa Kijiji cha SOS Zanzibar baada ya kukabidhi msaada wa vyakula kwa Watoto hao wanaoishi katika Kijiji hicho.



Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Familia ya beki wa kimataifa wa Ufaransa, Mamadou Sakho anayechezea Liverpool ya England jana jioni ametembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha SOS kilichopo Mombasa Unguja.

Sakho amefatana na mke wake Madna na Watoto wake wawili wa kike.
Juzi Ijumaa saa 3:00 za usiku katika uwanja wa Amaan Sakho amezindua Mashindano ya COCO SPORTS NDONDO CUP katika uwanja wa Amaan, mchezo ambao Taifa ya Jang’ombe walifungwa 2-1 na Mlandege SC.

Sakho yupo hapa Viswani Zanzibar tangu Jumamosi June 17, 2017 kwa ziara ya kiutalii ambapo awali ziara hiyo alianzia Tanzania bara kisha kurejea nyumbani Ufaransa na badae moja kwa moja Jumamosi kufika hapa Zenj.

Habari kwa hisani ya ZanziNews

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni