Mchezaji Leon Goretzka amefunga
magoli mawili ndani ya dakika nane za mwanzo wa mchezo wakati
Ujerumani ikiifunga Mexico magoli 4-1 katika dimba la Sochi na kukata
tiketi ya kuchuana na Chile katika fainali ya Kombe la Mabara.
Kiungo huyo wa Schalke alifunga goli
la kwanza akinasa pasi ya Benjamin Henrichs na kufunga kwa umbali wa
yadi 20 na kisha baadaye kuongeza goli la pili kupitia pande
alilopenyezewa na Timo Werner.
Werner baadaye akaifungia Ujerumani
goli la tatu kupitia pasi ya Jonas Hector, kabla ya Marco Fabian kufunga kiufundi goli
pekee la Mexico kwa shuti kali la umbali wa yadi 35. Amin Younes
kuongeza goli la nne la Ujerumani.
Leon Goretzka akifunga goli lake la kwanza katika mchezo wa jana
Amin Younes akifunga goli la nne la Ujerumani na kupigilia msumari wa mwisho
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni