Mshambuliaji wa Barcelona Lionel
Messi amekubali kuongeza mkataba na klabu hiyo utakaomfanya aendelee
kuwapo hadi mwaka 2021.
Messi, 30, ambaye alijiunga na
Barcelona tangu akiwa na umri wa miaka 13 ametia saini makubaliano
hayo aliporejea kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.
Uamuzi huo wa Messi umeshusha presha
za mashabiki wa Barcelona, ambapo katika mkataba mpya atalipwa kitita
cha paundi 500,000 kwa wiki.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni