Shaaban Dede enzi za uhai wake
Mwanamuziki nguli wa muziki wa dansi nchini Tanzania, Shaaban Dede amefariki dunia asubuhi ya leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu, Hamad Dede aliyekuwa akimuuguza baba yake, amesema baada ya kutokea kwa msiba huo mkubwa, familia itakutana na kupanga taratibu za mazishi baadaye.
Shaaban Dede ni mmoja wa wanamuziki mahiri walioutendea haki muziki wa dansi nchini kwa umahiri wake wa kuimba pamoja na utunzi. Mbali ya kuitumikia Msondo Ngoma Music Band hadi umauti yanamkuta, Dede aliwahi kuimba kwa mafanikio makubwa katika bendi za Ddc Mlimani Park, Bima Lee, Safari Sound na Tanzania All Stars.
Baadhi ya nyimbo alizotunga na kupata umaarufu mkubwa ni pamoja na Fatuma akiwa na Msondo Ngoma, Shangwe ya Harusi akiwa na Bima Lee, Talaka Rejea akiwa na Ddc Mlimani Park pamoja nawimbo wa Nyumba ya Mgumba haina Matanga akiwa na Safari Sound.
Rweyunga Blog inatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu mzito.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni