.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 6 Julai 2017

SERIKALI YAPATA GAWIO LA SHILINGI BILIONI 10 KUTOKA TAASISI ZA UMMA ILIZOWEKEZA HISA ZAKE

unnamed
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya TPB Profesa Lettice Rutashobya (kulia) akimkabidhi hundi kifani yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 1.032/- Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Phillip Mpango. Gawio hilo limetolewa kwa Serikali baada ya benki hiyo kupata faida ya shilingi Bilioni 15 mwaka jana. Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dorothy Mwanyika na wa pili kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Sabasaba Moshingi. Tukio hilo ilifanyika kwenye Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Dodoma.
1
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya TPB Profesa Lettice Rutashobya (kulia) akikabidhi hundi kifani yenye thamani ya shilingi Milioni Tisini na Saba kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Kanali Mstaafu Dkt. Haruni Kondo kwenye tukio la kukabidhi gawio kwa wanahisa wa benki hiyo. Akishuhudia ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Philip Mpango. Wa pili kulia ni Meneja wa Shirika la Posta Mkoa wa Dodoma Thobias Lawrence na Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Deogratius Kwiyukwa.
2
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, akisisitiza jambo wakati Benki ya Posta (TPB Bank Plc) ilipokabidhi Serikalini gawio la shilingi bilioni 1.032 kwa mara ya kwanza Mjini Dodoma.
4
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Puma, Dkt. Ben Moshi (Kulia), akimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, hundi kifani ya shilingi bilioni 7, ikiwa ni gawio la Kampuni hiyo baada kupata faida kwenye biashara ya kuuza mafuta mwa ka fedha uliopita. katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Philipe Corsaletti, tukio lililofanyika mjini Dodoma
5
Meneja wa Kampuni ya Kuhifadhi Mafuta-Tiper, Bw. Emmanuel Kondi, akipeana mkono na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango baada ya Kampuni yake kutoa gawio la shilingi bilioni 2 Serikalini, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Mjini Dodoma. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tiper Bw. Stephane Gay.
6
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya TPB Profesa Lettice Rutashobya (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Sabasaba Moshingi wakipiga makofi wakati Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akitoa nasha zake, wakati Benki hiyo ilipokabidhi hundi kifani yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 1.032/- ikiwa ni gawio lao kwa Serikali inayomiliki hisa 86.17 katika Benki hiyo. Tukio hilo ilifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Dodoma.
3 7
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania, Dkt. Haruni Kondo akisisitiza jambo wakati akiishukuru Banki ya TPB kwa kulipatia shirika lake gawio la shilingi milioni 97.6 baada ya Benki hiyo kupata faida.
8
                                                                               Na Benny Mwaipaja, WFM-Dodoma
 
SERIKALI imepokea gawio la zaidi ya shilingi bilioni 10 kutoka taasisi tatu ikiwemo TPB bank, na kampuni mbili za mafuta za Tiper na Puma ambazo serikali inamiliki hisa zake.

Taasisi ya kwanza kuwasilisha gawio hilo kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango mjini Dodoma ni Benki ya TPB ambayo mwenyekiti wake Profesa Lettice Rutashobya amekabidhi hundi kifani ya shilingi bilioni 1.032, ikifuatiwa na Kampuni ya kuhihadhi mafuta ya Tiper iliyowasilisha gawio la shilingi bilioni 2.

Kampuni ya mafuta ya Puma ikahitimisha zoezi hilo kwa kukabidhi hundi kifani ya shilingi bilioni 7 ambazo ni sehemu ya faida ya shilingi bilioni 14 ambazo kampuni hiyo imepata baada ya kulipa kodi.

Akizungumza katika tukio hilo lililofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Mjini Dodoma, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amezipongeza taasisi hizo na amezitaka Taasisi za Serikali na mashirika ya umma kuilipa Serikali gawio la hisa zake na zijiendeshe kwa ufanisi na kwa faida ili makusanyo hayo yaweze kuwahudumia wananchi.

Dkt. Mpango amerejea kauli yake aliyoitoa bungeni mjini Dodoma wakati akiwasilisha Bajeti Kuu kwamba Serikali itatoa kipaumbele kwa kufanya biashara na taasisi zake za Umma ili ziweze kujiimarisha kimapato na hatimaye kutoa gawio Serikalini.

“Leo ni siku nzuri sana kwa watanzania kwa sababu Serikali inapokea gawio la shilingi bilioni 10 kwa niaba yao lakini fedha hizi hazitoshi nataka mfanye vizuri zaidi ili gawio liweze kuongezeka ili tuzielekeze kutatua kero zinazoikabili jamii ikiwemo elimu, afya na maji” alilisisitiza Dkt. Mpango.

Katika tukio hilo pia, Benki ya TPB Plc imelipatia Shirika la Posta kiasi cha shilingi milioni 97.8 ikiwa ni gawio kulingana na hisa zake asilimia 7.98 inazomiliki katika Benki hiyo.

Akipokea hundi kifani ya kiasi hicho cha gawio, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta nchini, Dkt. Haruni Ramadhan Kondo, ameiomba Serikali ililipe shirika lake kiasi cha shilingi bilioni 3.6 ambazo ni malipo ya pensheni ya wastaafu wa lililokuwa Shirika la Posta na Simu la Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo Shirika limelipa pensheni hizo kwa niaba ya Serikali ili liweze kuongeza mtaji na kujiendesha kwa faida zaidi.

Awali Wenyeviti wa Bodi za wakurugenzi wa Taasisi hizo wameahidi kuendelea kufanya biashara kwa umahili mkubwa ili kuongeza gawio kwa wanahisa wake na kuiomba iwawekee mazingira yatakayosaidia kufanikisha azma yao hiyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPB Bank, Profesa Lettice Rutashobya, amesema kuwa Benki yake imeendelea kukua kwa kasi, kuimarika na kufanya vizuri katika biashara ya fedha pamoja na kuwa mahili katika ubunifu na kuwa tishio kwa taasisi nyingine za fedha.

Nae Meneja wa Kampuni ya Kuhifadhi Mafuta-Tiper, Bw. Emmanuel Kondi, ameiomba Serikali kuiwezesha kampuni hiyo kufanya biashara kwa mafanikio zaidi hivyo kuongeza gawio ikiwemo kuangalia upya mfumo wa himaya moja ya Forodha ambao amesema pamoja na kuwa na ufanisi mkubwa una baadhi ya changamoto.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Kuuza Mafuta-Puma, Dkt. Ben Moshi amesema kuwa Kampuni yake ilitengeneza faida na kuiwezesha kutoa gawio la shilingi bilioni 7 kwa Serikali ikilinganishwa na shilingi bilioni 4.5 ilizotoa mwaka wa fedha uliopita.

Utaratibu wa Taasisi za Serikali na mashirika ya umma kulipa gawio la hisa kwa Serikali na wanahisa wengine ni maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ya kuhakikisha kuwa Taasisi hizo zinafanya kazi kwa ufanisi, kuzalisha faida na kutoa gawio kwa Serikali ili mapato hayo yaweze kuhudumia wananchi katika Nyanja mbali mbali kama vile huduma za afya, elimu, maji na barabara.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni