.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 3 Julai 2017

UJERUMANI YATWAA KWA MARA YA KWANZA KOMBE LA MABARA

Mabingwa wa dunia Ujerumani wametwaa kwa mara ya kwanza Kombe la Mabara dhidi ya mabingwa wa Copa Amerika Chile baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

Katika mchezo huo wa fainali alikuwa mchezaji Lars Stindl aliyefunga goli pekee katika dakika ya 20 kufuatia makosa ya Marcelo Diaz.

Katika mchezo huo ambao Chile walionekana kuutawala kwa muda mwingi wachezaji wake Arturo Vidal na Angelo Sagal wote mashuti yao yalipaa nje ya ngoli.

Awali katika kusaka mshindi wa tatu wa mashindano hayo Adrien Silva alifunga penati katika dakika za ziada na kuifanya ureno kuibuka na ushindi wa magoli 2- dhidi ya Mexico.
     Wachezaji wa Ujerumani wakishangilia ushindi huku mmoja wao akilibusu kombe
Kocha wa Ujerumani Joachim Low akiwa ameshika kombe la mabara pamoja na mchezaji wake

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni