Arsenal imetwaa ngao ya jamii baada
ya kuibuka na ushindi wa magoli 4-1 kwa mikwaju ya penati, kufuatia
kumaliza dakika 90 zikiwa na matokeo ya goli 1-1 dhidi ya Chelsea.
Katika mchezo huo ulioshuhudia Pedro
akipewa kadi nyekundu dakika 10 kabla ya mchezo kuisha Chelsea
walipata goli la kwanza kupitia Victor Moses na Sead Kolasinac
alisawazisha kwa kichwa.
Katika mikwaju ya penati kipa
Thibaut Courtois alipaisha juu penati aliyoipiga huku mchezaji mpya
Alvaro Morata aliyesajiliwa kwa paundi milioni 55 naye akikosa
penati.
Olivier Giroud alifunga penati ya
ushindi na kuifanya Arsenal inayonolewa na Arsene Wenger kuanza msimu mpya kwa kutwaa ngao ya
jamii.
Victor Moses akifunga goli la kwanza katika mchezo huo
Sead Kolasinac akiruga juu kupiga kwa kichwa mpira uliosawazisha goli
Mchezaji wa Chelsea Pedro akipewa kadi nyekundu na refa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni