.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 17 Agosti 2017

IGP SIRRO AKUTANA NA BALOZI WA KOREA KUSINI SONG GEUM YOUNG

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na Balozi wa Korea Kusini Song, Geum Young wakati wa siku maalum ya kuadhimisha urafiki kati ya Tanzania na nchi ya Korea kusini ambapo Balozi huyo amekubali kusaidia kufunga kamera maalum za kufuatilia wahalifu-CCTV katika jiji la Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Korea Kusini Song, Geum Young (wa tatu kutoka kushoto) pamoja na maofisa wengine wakati wa siku maalum ya kuadhimisha urafiki kati ya Tanzania na nchi ya Korea kusini ambapo Balozi huyo amekubali kusaidia kufunga kamera maalum za kufuatilia wahalifu-CCTV katika jiji la Dar es Salaam.
Kamishna wa Polisi, Oparesheni na Mafunzo Nsato Marijani akizungumza na Askari Polisi wanaokwenda kwenye Operesheni ya ulinzi wa amani Darfur Sudan wakati wa zoezi la kuwakabidhi bendera ya taifa ambapo jumla ya Askari 24 wanatarajia kuondoka hivi karibuni.
Kamishna wa Polisi, Oparesheni na Mafunzo Nsato Marijani akiwakabidhi bendera ya taifa Askari Polisi wanaokwenda kwenye Operesheni ya ulinzi wa amani Darfur Sudan ambapo jumla ya Askari 24 wanatarajia kuondoka hivi karibuni.(Picha na Jeshi la Polisi)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni