Timu ya Real Madrid imeifunga Barcelona 2-0 katika dimba la Bernabeu
na kutwaa kombe la Hispania la Super Cup kwa ushindi wa jumla wa magoli 5-1.
Mabingwa hao wa Hispania na Ulaya waliutawala mchezo huo
wakicheza bila ya nyota wao Cristiano Ronaldo anayetumikia adhabu ya
kutokucheza michezo mitano.
Marco Asensio, aliyefunga katika ushindi wa magoli 3-1 katika
mchezo wa kwanza, aliipatia Real Madrid goli la kwanza kwa shuti la umbali wa yadi
25.
Karim Benzema aliinasa krosi ya Marcelo na kumgeuza beki Samuel
Umtiti na kuipatia Real Madrid goli la pili huku Barcelona wakishindwa kabisa
kufurukuta.
Cristiano Ronaldo akiwa anashangilia ushindi huku akiwa ameshika kombe
Lionel Messi akiwa na baadhi ya wachezaji wenzake wa Barcelona wakiwa hoi wasijue la kufanya baada ya kipigo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni