Bondia Anthony Joshua atatetea
mikanda yake ya IBF na WBA ya uzito wa juu duniani dhidi ya Carlos
Takam baada ya bondia Kubrat Pulev kujitoa kutokana na kuwa majeruhi.
Pambano lao hilo limepangwa
kufanyika Oktoab 28 katika uwanja wa Cardiff huku tiketi zaidi ya
70,000 zikiwa zimeshauzwa.
Pambano hilo litakuwa la kwanza kwa
Joshua tangu amdunde Wladimir Klitschko katika dimba la Wembley mwezi
April, na kuongeza mkanda wa WBA huku akitetea wa IBF alioutwaa 2016.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni